09. Kuritadi kwa kuwa na mashaka


04- Kukufuru kwa shaka: Akiweka shaka moyoni mwake, je, yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni sahihi au sio sahihi? Je, kuna kufufuliwa au hakuna? Je, kuna Pepo na Moto au hakuna kitu? Huyu anakufuru kwa shaka yake hata kama anaswali, anafunga na anafanya matendo mengine. Akiwa si mwenye uhakika kwa imani, kwa msemo mwingine ana mashaka juu ya usahihi wa yale yaliyokuja nayo Mitume na anaona yanaweza kuwa sahihi kama ambavo vilevile yanaweza kuwa si sahihi, huyu anazingatiwa ni mwenye karitadi kutoka katika dini ya Uislamu. Haijalishi kitu hata kama atakuwa anashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume Wake. Lakini hata hivyo sisi hakuna tunachotazama isipokuwa yale ya dhahiri. Ama kuhusu yale yaliyomo ndani ya nyoyo katika yakini na shaka, mani na kufuru, haya hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 24
  • Imechapishwa: 06/05/2018