Nimetumia chapa zifuatazo wakati nilipokuwa nikimnukuu Sayyid Qutwub:

1 – Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan, chapa ya 13, 1407, Daar-ush-Shuruuq.

2 – at-Taswiyr al-Fanniy fiyl-Qur-aan, chapa ya 10, 1408, Daar-ush-Shuruuq.

3 – al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah, chapa ya 12, 1409, Daar-ush-Shuruuq.

4 – al-´Adaalah al-Ijtimaa-´iyyah, chapa ya 5[1].

5 – Nahuu Mujtama´ Islaamiy, chapa ya 8, 1408, Daar-ush-Shuruuq.

6 – Ma´rakat-ul-Islaam war-Ra’smaaliyyah, chapa ya 10, 1408, Daar-ush-Shuruuq.

7 – as-Salaam al-´Aalamiy wal-Islaam, chapa ya 8, 1399, Daar-ush-Shuruuq.

8 – Ma´aalim fiyt-Twariyq, chapa ya 15, 1412, Daar-ush-Shuruuq.

Hizi ndio chapa za vitabu vya Sayyid Qutwub nilizotumia katika kitabu changu “Adhwaa´ Islaamiyyah”. Zote ni chapa zilizokuja nyuma. Tukifuata madai ya Shaykh Bakr na kwamba chapa zilizokuja nyuma zinafuta zile za kale, basi nitakuwa nimetumia zile chapa zilizofutwa zilizokuja nyuma.

Ninaapa kwa Allaah napendelea kuanguka kutoka mbinguni kuliko kumsemea uongo Allaah au muislamu yeyote. Naapa kwa Allaah napendelea kuanguka kutoka mbinguni au kufa mara elfu moja kuliko kumfanyia khiyana kafiri, sembuse tusizungumzie muislamu, au kutokuwa na uaminifu katika kunukuu na elimu.

[1] Nimeoanisha kati ya chapa hizi mbili kubainisha kuwa Sayyid Qutwub hakujirejea kabisa makosa yake kwa ´Uthmaan na kule kurekebisha baadhi ya ibara, ambazo ni chache mno, hazibadilishi chochote katika uhalisia wa mambo.