09. Ameona damu kipindi cha funga lakini hana uhakika kama ni hedhi


Swali 9: Ni ipi hukumu ya funga ya mwanamke akiona damu lakini asiwe na uhakika kama ni damu ya hedhi?

Jibu: Funga ya siku yake hiyo ni sahihi. Kwa sababu msingi ni kutokuwepo kwa hedhi mpaka imbainikie kwamba ni hedhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 12
  • Imechapishwa: 18/06/2021