8- Hawaitilii umuhimu wowote ´Aqiydah ya Kiislamu sahihi ambayo ndio msingi wa dini. Kwa sababu ya ujinga huu, na vilevile sababu nyenginezo, utaona namna walivyochanganya. Mmoja ni Suuniy, mwingine ni Shyi´iy, baadhi ya wengine ni waabudu makaburi. Kinachowakusanya ni nidhamu ya pote kikamilifu. Kwa mujibu wa hilo kunaundwa udugu, kunusuriana na kusaidiana. Hili ni balaa kubwa kwelikweli.[1]

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

 

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 25/03/2017