08. Uislamu unafahamika kwa Wahy, sio kwa akili

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

”Haifahamiki kwa akili wala matamanio. Inahusiana tu na kufuata na kuacha matamanio.”

MAELEZO

Shari´ah ya Kiislamu haifaamiki kwa kutumia akili, isipokuwa tu ni nukuu ambazo ni lazima kuzifuata. Kwa msemo mwingine yale yaliyosemwa na Allaah na mapokezi Swahiyh kutoka kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hayo ndio lazima kuyafuata. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ameamrisha hilo pale aliposema:

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ

“Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu na wala msifuate badala Yake walinzi wengine – ni machache mnayoyakumbuka.”[1]

Yale tuliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wetu ni Qur-aan na Sunnah. Vyote viwili ni Wahy kutoka kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Hivyo ni lazima kufuata Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu sahihi na wa salama. Haijuzu kuzusha. Haijuzu kuwafuata watu wa matamanio na watu wa upotevu. Kwa sababu matamanio, upotevu na uzushi vyote ni shari kwa mwenye navyo kwa sababu vinaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Uhai mzuri na uliobarikiwa ni ule uliyoko chini ya kivuli cha Shari´ah ya Allaah; Kitabu cha Allaah kitukufu na Sunnah safi za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 07:03

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 55
  • Imechapishwa: 02/10/2019