08. Sura ya pili: Mitazamo ya nyumati zilizopotea katika mlango wa uola na kuiraddi mitazamo hiyo

2- Allaah amewaumba viumbe wakiwa na maumbile ya Tawhiyd na kumtambua Mola na Muumbaji (Subhaanah). Allaah (Ta´ala) amesema:

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ

“Basi elekeza uso wako katika dini yenye kujiengua na upetevu inayoelemea haki. Umbile la asili la kumpwekesha Allaah aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah.”[1]

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا

“Pindi Mola wako alipowaleta katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao, kizazi chao, akawashuhudisha juu ya nafsi zao: “Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia!”[2]

Kukubali uola wa Allaah na kuelekea Kwake ni jambo la kimaumbile. Shirki ni kitu kilichozuka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila mtoto huzaliwa katika maumbile. Baadaye wazazi wake ndio humfanya akawa myahudi, akawa mnaswara au akawa mwabudu moto.”[3]

Lau mtu angeachwa na maumbile yake basi angelielekea katika Tawhiyd na angelikubali ulinganizi wa Mitume waliokuja nao, kukateremshwa vitabu kwa ajili yake, ukafahamishwa na alama za kilimwengu. Lakini hata hivyo malezi mabaya na mazingira ya kikafiri ndivo ambavyo hubadilishwa mwelekeo wa mtoto. Matokeo yake mtoto

Allaah (Ta´ala) amesema katika Hadiyth ya kiungu:

“Nimewaumba waja Wangu wakiwa ni wapwekeshaji. Wakabadilishwa na mashaytwaan.”[4]

Bi maana wakawageuza kwenda katika kuyaabudu masanamu na kuyafanya ni waungu badala ya Allaah. Matokeo yake wakatumbukia katika upotevu, upoteaji, kufarikiana na kutofautiana; kila mmoja anajifanyia mola anayemwabudu mbali na mola wa huyo mwengine. Kwa sababu pindi walipomwacha Mola wa kweli ndipo wakapewa mtihani wa kujichukulia waungu wa batili. Amesema (Ta´ala):

فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ

“Basi huyo ndiye Allaah, Mola wenu wa haki, kuna nini baada ya haki isipokuwa upotevu?” [5]

Upotevu hauna kipimo wala kikomo. Ni jambo ambalo halina budi kwa kila yule atayempa mgongo Mola wa haki. Amesema (Ta´ala):

أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا أَسْمَاءً سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ

“Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja pekee, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, asiyepingika? Hamwabudu badala Yake isipokuwa majina tu mmeyaita nyinyi na baba zenu; hakuyateremshia Allaah kwayo hoja yoyote.”[6]

[1] 30:30

[2] 07:172

[3] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[4] Muslim (2865).

[5] 10:32

[6] 12:39-40

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 23/01/2020