08 – Rabiy´ al-Madkhaliy anatumia chapa za zamani za vitabu vya Sayyid Qutwub

Shaykh Bakr amesema:

“Hapa kunafuata dalili:

1- Nimeona kuwa kumetumiwa chapa za zamani za vitabu vya Sayyid Qutwub, kama “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” na “al-´Adalah al-Ijtimaa´iyyah”. Wewe mwenyewe unajua, kama ilivyo kwa mfano katika hashiya (maelezo ya chini) ukurasa wa 29, ya kwamba vina chapa mpya, zilizosahihishwa. Katika hali hii ni wajibu kurejea katika ile chapa ya mwisho ya kila kitabu kwa sababu marekebisho ya mwisho yanafuta yale makosa yaliyotangulia. Hili unalijua. Lakini kuna uwezekano ikawa ni kosa la mwanafunzi aliyekujia na taarifa hizi bila ya wewe kujua hilo.”

Ee Shaykh! Umejiingiza katika kitu ambacho ni mjinga kwacho kabisa[1]. Inaonekana kuwa hujui ni I´tiqaad na fikira zipi alizokuwa nazo Sayyid Qutwub na ni chapa zipi zilizo na vitabu vyake wala ni chapa zipi nilizotumia wala kama Sayyid Qutwub alirekebisha makosa au hakurekebisha. Ni mjinga wa yote hayo kabisa. Na wala hukufikiria yanayopelekea katika matokeo ya madhara ya mashambulizi haya.

Hivi kweli ulisoma kitabu changu “Adhwaa´ Islaamiyyah” kwa umakini na utulivu na kuona nukuu zake na kisha kurejea katika chapa ya vitabu vya Sayyid Qutwub vya zamani na vilivyokuja baadae? Hivi kweli umehakikisha kuwa nimepanga kurejea katika chapa za zamani, zilizofutwa na kutumia chapa zilizofutwa zilizokuja baadae ili kuzinasibisha I´tiqaad na fikira za Sayyid Qutwub ambazo ametubia kwazo? Ikiwa unamaanisha hayo, basi ni lazima uyathibitishe kwa kubainisha chapa mbalimbali zilizotumiwa, kurasa, tarehe ya uchapishaji na maneno yaliyofutwa ambayo Sayyid Qutwub ametubia kwa Allaah katika yale aliyoandika katika chapa zilizokuja nyuma pale ambapo kwa mfano anamtukana ´Uthmaan na kuangusha ukhalifah wake katika kitabu “al-´Adaalah”, kuzikanusha sifa za Allaah katika “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” na “Taswiyr al-Fanniy”, kuzungumza kwa ujamaa katika “al-´Adaalah” na “Ma´rakat-ul-Islaam war-Ra´smaaliyyah”, kuukufurisha Ummah katika “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”, “al-´Adaalah”, “al-Islaam wa Mushkilaat-ul-Hadhwaarah”, kuzungumza kwa nadharia ya viumbe vyote ni Allaah katika “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” na kadhalika.

Hutoweza kufanya hivo si wewe, al-Ikhwaan al-Muslimuun, Qutbiyyuun wala mapote mengine yote ya kipotevu ambayo yanamtukuza Sayyid Qutwub hayawezi kuthibitisha kuwa mimi nimetumia chapa za kale, zilizofutwa au kwamba Sayyid Qutwub alijirejea katika Bid´ah na upotevu wake ambao umesheheni kwenye vitabu vyake.

[1] Nayasema haya kujengea ya kwamba yeye mwenyewe amesema kuwa hajasoma vitabu vya Sayyid Qutwub. Lakini kama ameshavisoma vitabu vya Sayyid Qutwub kisha ananificha, basi yeye mwenyewe ndiye mwenye jukumu ya hilo.