Swali 08: Sisi ni jopo la wafanyikazi ambao tunafanya kazi katika idara ya serikali ambayo iko na wafanyikazi karibu thelathini na tunaswali kwenye Muswallaa wa idara nyuma ya msimamizi wa idara. Baadhi ya wenzetu hawaswali pamoja nasi badala yake wanaswali msikitini ambao uko karibu nasi takriban mita 300. Ni upi usawa? Tuswali katika Muswallaa au twende kuswali msikitini pamoja na mkusanyiko. Msimamizi alipoambiwa amesema wakienda msikitini pengine wakachelewa kurudi katika kazi zao[1].

Jibu: Ni lazima kwa watu mfano wenu kuswali msikitini pamoja na ndugu zenu waislamu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayesikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”[2]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) aliulizwa ni nini udhuru ambapo akasema: “Khofu au maradhi.”

Ameipokea Ibn Maajah, ad-Daaraqutwniy, Ibn Hibbaan na al-Haakim kwa cheni ya wapokezi Swahiyh ilio na sharti za Muslim.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati alipoulizwa na bwana mmoja kipofu kwamba hana kiongozi wa kumwongoza kuelekea msikitini. Je, ninayo ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuuliza: “Je, wasikia wito wa swalah?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Basi imewajibika.”[3]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Zipo Hadiyth nyingi zenye maana kama hii.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/62-63).

[2] Ibn Maajah (785).

[3] Muslim (653) na an-Nasaa´iy (850).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 33-35
  • Imechapishwa: 25/11/2021