08. Je, mtu achanganyike na makundi mbalimbali au awakate?


Swali 8: Je, mtu achanganyike na makundi mbali mbali au awasuse?

Jibu: Ikiwa mtu yuko na elimu na umaizi[1] na akachanganyika nao kwa lengo la kuwalingania katika Sunnah na kuacha kosa, ni jambo zuri. Ni aina ya kulingania katika dini ya Allaah. Ama ikiwa mtu anachanganyika nao ili atangamane nao na kuwa na urafiki nao bila ya kuwalingania na kuwabainishia, haijuzu.

Haijuzu kwa mtu kuchanganyika na waendaji kinyume ikiwa hilo halileti faida ya Kishari´ah kwa aina ya kuwalingania katika Uislamu sahihi na kuwabainishia haki ili waweze kurejea[2]. Mfano wa hilo ni kama jinsi Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) alivoenda kwa watu wa Bid´ah Msikitinii na kuwakemea kwa Bid´ah zao. Mfano mwingine ni Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alivowaendea Khawaarij na kujadiliana nao na kuzivunja shubuha zao. Kuna ambao walijirejea.

Ikiwa kuchanganyika nao ni kwa lengo hili ni sawa. Lakini wakiendelea kushikamana na upotevu wao ni wajibu kujiepusha nao na kupambana nao katika njia ya Allaah.

[1] Hili ni sahihi kwa nisba ya watu. Ni jambo linalowezekana kuwalingania na kuwaathiri. Hata hivyo ni jambo lisilowezekana kwa jumla kubadili mfumo na viongozi wao. Badala yake wao ndio wanaoweza kumuathiri yule mwenye kuchanganyikana nao bila ya wao kuathirika. Inapokuja katika Da´wah yenyewe, kwa jumla mapote haya hayaachi mafundisho ya viongozi wao. Mfano wa mapote haya ni al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Ni nasaha ngapi wameshapata kutoka kwa watu wakweli! Ni mara ngapi kumeandikwa juu yao! Pamoja na yote haya bado wamesimama pale pale. Hapa una dalili ya niyasemayo. Muasisi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Hasan al-Bannaa amesema chini ya kichwa cha khabari “Mawqiyfunaa min ad-Daw´aat”:

“Msimamo wetu juu ya Da´wah nyinginezo ni sisi tunazipima kwa mizani ya Da´wah yetu; yale yanayoafikiana nayo tunayakaribisha na yale yasiyoafikiana nayo sisi ni wenye kujiweka nayo mbali.” (Majmuu´-ur-Rasaa-il, uk. 24)

Ee Allaah! Shuhudia ya kwamba mimi ni mwenye kujiweka mbali na Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun na muasisi wake. Ni wenye kwenda kinyume na Qur-aan, Sunnah na mfumo wa Salaf.

Kutokana na haya wao hawakubali Da´wah ya yeyote. Kwa sababu wao wanachotaka ni Da´wah za wengine zifuate Da´wah yao na ziwe chini yao – na Allaah ndiye Anajua zaidi.

[2] Ikiwa mtu kikweli amelazimika kuchanganyika nao ili kuwalingania katika mfumo wa Salaf, ni wanachuoni tu au wanafunzi walio imara katika ´Aqiydah sahihi, Sunnah na mfumo wa Salaf ndio wanaotakiwa kufanya hivo na si mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 18/02/2017