d) Ni haramu kwa mwanamke kufanya chanjo [tattoo] kwenye mwili wake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kufanya chanjo na mwenye kufanywa chanjo. Mwanamke mwenye kufanya chanjo ni yule anayechoma mkono au uso wake kwa sindano kisha anatia pahali hapo palipochanjwa wanja au wino. Huyo mwanamke mwingine ni yule anayefanyiwa jambo hilo. Kitendo hichi ni haramu na ni dhambi kubwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani yule mwenye kufanya hivo au mwenye kufanyiwa. Mtu halaaniwi isipokuwa kwa kufanya moja katika madhambi makubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat ´alaa Ahkaam Takhtasswu bil-Mu´minaat, uk. 22
  • Imechapishwa: 23/10/2019