08. Hadiyth ”Yule ambaye atatawadha mfano wa wudhuu´ wangu huu… “

183 – Amesimulia tena:

“Aliletewa maji ya kutawadha kipindi ambapo alikuwa ameketi chini. Akatawadha na akafanya vizuri wudhuu´ wake kisha akasema: “Nilimwona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha hali ya kuwa ameketi mkao huu. Akafanya vizuri wudhuu´ wake kisha akasema: ”Yule ambaye atatawadha mfano wa wudhuu´ wangu huu, kisha akaenda msikitini na akaswali Rak´ah mbili halafu akaketi chini, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na wengine.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/190)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy