07. Wachangamfu katika Bid´ah, wazembeaji katika faradhi


Miongoni mwa mambo yanayoshangaza ni kwamba watu wengi wanapata uchangamfu na kujipinda katika kuhudhuria mazazi haya yaliyozuliwa, kuyatetea na wanaacha yale ambayo Allaah amewajibisha katika kuhudhuria swalah za ijumaa na swalah za mkusanyiko, hawayapi umuhimu na wala hawaoni kuwa wamefanya maovu makubwa. Hapana shaka kuwa hayo ni kutokana na unyonge wa imani, uchache wa utambuzi na dhambi nyingi zilizoukumba moyo katika aina mbalimbali ya madhambi na maasi. Tunamwomba Allaah afya sisi na waislamu wengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 12
  • Imechapishwa: 12/01/2022