Haya yanatakiwa kutambulika. Mapote yote, ya zamani na ya sasa, ni wenye kutilia mkazo Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Kwa mujibu wao wanaona kuwa mja anakuwa muislamu kwa sababu tu anakubali kuwa Allaah ndiye Muumbaji na Mruzukaji. Hivo ndivo wameandika ´Aqiydah zao kwenye vitabu. Vitabu vya wanafalsafa vinazungumzia tu Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na dalili zake. Haya hayatoshi. ´Ibaadah ni jambo la lazima. Amesema (Ta´ala):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

”Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [waungu batili].”[1]

Wakiwaamrisha watu kumwabudu Allaah. Hii ndio Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”[2]

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

“Mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe Yeye na chochote.”[3]

Aayah zote zinaamrisha na kuita katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Mitume wote walilingania katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah, wakawaamrisha nyumati zao na wakawakataza shirki. Hili ndilo kusudio na lengo la Tawhiyd.

Ama kuhusu Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat, inapingwa na wazushi kama Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah pamoja na kutofautiana kwao katika jambo hilo.

[1] 16:36

[2] 21:25

[3] 04:36

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 04/06/2019