07. Sura ya pili: Ufahamu wa neno ´Mola` ndani ya Qur-aan na Sunnah

1- Neno ´Mola` halitumiki kwa kuachilia isipokuwa kwa Allaah (Ta´ala) ambaye anasimamia yanayoendana na viumbe. Mfano wa maneno Yake:

رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Mola wa walimwengu.”[1]

رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ

“Mola wenu na Mola wa baba zenu wa mwanzo.”[2]

Jina hilo halitumiki kwa wengine isipokuwa kwa kiambatanisho chenye mipaka. Kama inavosemwa baba mwenye nyumba (رب الدار), mwenye farasi (ربُّ الفرس‏). Miongoni mwake ni maneno Yake (Ta´ala) akisimulia kuhusu Yuusuf (´alayhis-Salaam):

اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ

“Nikumbuke mbele ya bwana wako (رَبِّكَ ). Lakini shaytwaan alimsahaulisha kumkumbuka kwa bwana wake.”[3]

Kutokana na moja ya maoni katika kuifasiri Aayah hiyo[4]. Maneno Yake (Ta´ala):

وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ

”Mfalme akasema:  “Nileteeni [naye huyo Yuusuf]. Basi alipojiwa na mjumbe alisema: “Rejea kwa bwana wako.”[5]

 أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا

”Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake (رَبَّهُ) mvinyo.”[6]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu yule mtu aliyempoteza ngamia wake:

“… mpaka atapompata bwana wake (ربها‏).”[7]

Kwa haya imepata kubainika kwamba Mola hutumika kwa njia ya uhakika na isiyokuwa na uhakika. Kwa hivyo inasemwa Mola, Mola wa walimwengu au Mola wa watu. Jina la Mola halitumiki kwa mwengine asiyekuwa Allaah isipokuwa kwa njia isiyokuwa ya uhakika. Kwa mfano baba wa nyumba (رب الدار), baba mwenye nyumba (رب المنزل) na mwenye ngamia (رب الإبل).

Maana ya Mola wa walimwengu ni muumbaji, mfalme wao, mwenye kuwatengeneza, mwenye kuwalea kwa neema Zake, kwa kuwatumiliza Mitume Wake, kuteremsha Vitabu Vyake na mwenye kuwalipa kwa matendo yao.  ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakika uola unapelekea kuwaamrisha waja na kuwakataza na kumlipa mwenye kufanya wema kwa wema wake na mwenye kufanya vibaya kwa ubaya wake.”[8]

Huu ndio uhakika wa uola.

[1] 01:02

[2] 26:26

[3] 12:42

[4] Tafsiyr ya Ibn Kathiyr (02/480).

[5] 12:50

[6] 12:41

[7] Ameipokea al-Bukhaariy (2428) na Muslim (31).

[8] Madaarij-us-Saalikiyn (01/68).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 23/01/2020