07. Mfano wa pili kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan

al-´Ayyaashiy (01/180) amesema:

“Habiyb as-Sijistaaniy amesema kuwa alimuuliza Abu Ja´far kuhusiana na Kauli ya Allaah:

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ

“Na Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii. [Akawaambia]: “Kwa niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah. Kisha [siku moja] atakujieni Mtume mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” (03:81)

Vipi Muusa ataamini kuwa ´Iysaa atamnusuru na hakukutana naye? Vipi ´Iysaa ataamini kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atamnusuru na hakukutana naye? Akajibu: “Habiyb! Kuna mengi yaliyoondoshwa kwenye Qur-aan na hakuna kilichobaki isipokuwa ni herufi tu zilizoandikwa kimakosa na wanaume wakapitishwa. Huu ndio uhakika wa mambo. Isome namna hii:

“Na Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii wa Ummah. [Akawaambia]: “Kwa niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah. Kisha [siku moja] atakujieni Mtume mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.”

Namna hii ndivyo iliyoteremshwa, ee Habiyb! Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hakuna Ummah wowote kabla ya Muusa uliotimiziwa fungamano ambalo Allaah Alilochukua kwa Manabii wao. Ummah ambao Muusa aliuendea ulimkadhibisha na hawakumuamini wala kumnusuru isipokuwa watu wachache. Ummah wa ´Iysaa ulimkadhibisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipowajia na hawakumuamini waka kumnusuru isipokuwa watu wachache. Ummah huu umekanusha fungamano ambalo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilochukua kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib siku ambayo alimteua kama kiongozi kwa watu na akawahimiza kuwa chini ya uongozi wake na kumtii wakati wa uhai wake na wakashuhudia kwa hilo juu ya nafsi zao. Ni fungamano lipi ambalo ni muhimu zaidi kuliko fungamano la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hawakulitekeleza. Bali walilikanusha na kulikadhibisha.”

Mhakikia ameelekeza katika “al-Bihaa”, “al-Burhaan” na “as-Swaafiy”.

1- Namna hii ndivyo wanafiki wanavyowatuhumu Maswahabah waaminifu na wa kweli wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba wameondosha kwenye Qur-aan Aayah nyingi. Hata hivyo Allaah Amewatakasa Maswahabah waaminifu wa Muhammd (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wanafiki ndio wenye kuongeza maongezo yao wenyewe, kuchocheka kwa chuki na unafiki. Kisha wanawatuhumu Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa wameondosha Aayah nyingi katika Qur-aan. Ole wao kwa wayasemayo. Isitoshe wanasema kuwa hapakubaki kwenye Qur-aan isipokuwa herufi tu zilizoandikwa kimakosa. Waongo wakubwa! Allaah Ameahidi kukihifadhi Kitabu Chake juu ya uongezaji na upunguzaji. Mkono ulio mchafu wa Baatwiniyyah ungeliweza kujaribu kuongeza au kupunguza, Allaah ambaye Ametimiza ahadi Yake Amewafedhehesha. Hivyo ndivyo alivyofanya kwa mfano wa hawa Raafidhwah Baatwniyyah.

2- Wanazusha uongozi kwa ´Aliy na kudai ya kwamba fungamano la uongozi huu ni muhimu zaidi kuliko fungamano Alilochukua Allaah kwa Manabii (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Halafu wanawatuhumu Maswahabah kuwa walifuta fungamano hili. Hii ndio sababu ya wao kuwakufurisha. Ni ubaya uliyoje wa yale wanayoyazusha!

Zingatia ambavyo hawataji fadhila yoyote inayohusiana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Manabii au mtu mwingine isipokuwa wanampachika ndani yake ´Aliy na familia yake. Wanaweza mpaka wakafanya wawashinde. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba si ´Aliy wala familia yake haiko radhi kwa uadui na chuki kama hii kwa Kitabu cha Allaah, Mtume Wake na waja wanaomuamini na kumcha.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 19/03/2017