07. Matendo maovu ya Juhaymaan Makkah ni mfano wa ugaidi

6- Kwa hivyo harakati za kigaidi na mbaya zinazofanywa na kundi dogo, la kshabiki na lililopindukia waliofeli kwa ndoto za kipumbavu na matumaini ya uongo ni mfano wa wazi wa kigaidi.

Kundi hili dogo liliingia msikiti Mtakatifu siku ya jumanne tarehe 1 Muharram mwaka 1400. Kulikuwa kuna kundi linaloitwa Mahdiy kutokamana na jina la Muhammad bin ´Abdillaah al-Qahtwaaniy. Alikuwa akifuatwa na kushaji´ishwa na msemaji wake Juhaymaan bin Sayf al-´Utwaybiy. Walikuwa na silaha na mabunduki. Chini ya khofu na vitisho vya kuuawa wakawataka waislamu kula kiapo kwa huyu anayedaiwa kuwa Mahdiy. Namna hii ndivyo wanavyotaamiliwa waislamu wote kwa ujumla na khaswa waswaliji katika msikiti Mtakatifu.

Ni damu ngapi walizomwaga kwa dhuluma na pasi na haki! Wanachuoni waliwaomba wahukumiwe kwa Shari´ah ya Allaah, lakini wakakataa na badala yake wakaendelea kung´ang´ania shari, usafi, dhambi, maasi na ukaidi. Matokeo yake majeshi ya Allaah mashujaa, majasiri na wanaume wapwekeshaji kutoka katika jeshi la kisaudi likawavamia. Wakawalazimisha kujisalimisha. Watu mia moja na sabini wakakamatwa wakiwa hai na wakahukumiwa kwa Shari´ah ya Allaah. Watu sitini na tatu wakahukumiwa kuuawa. Wengine waliobaki wakaadhibiwa kwa kutiwa jela na kuchapwa. Allaah akausafisha msikiti Mtakatifu kutokamana na kundi hili shambulizi na la magaidi.

Linalosikitisha sana ni kuwa wanajiita wao wenyewe “Jama´aat-ul-Hadiyth”. Hata kama wamezihifadhi baadhi ya Hadiyth hawaelewi maana yake kabisa. Migeuko inamrudilia yule yule mkandamizaji.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 03/04/2017