07. Maswahabah ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

na ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Yule asiyechukua kutoka kwao amepotea na kuzusha. Kila Bid´ah ni upotevu na upotevu na watu wake ni Motoni.

Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wale waliokuja baada yao ambao wamewafuata kwa wema ndio Ahl-us-Sunnah. Hawa ndio watu wenye kufuata njia sahihi. Hii ndio Sunnah anayopambanua hivi sasa. Nao vilevile ndio al-Jamaa´ah ya kihakika. Kuhusu kukusanyika kwa wengine juu ya mambo batili, hawa hawastahiki kuitwa al-Jamaa´ah. Haijalishi kitu hata kama itakuwa ni idadi ya watu wengi:

تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ

”Utawadhania wako pamoja, kumbe nyoyo zao ziko mbalimbali.” (59:14)

Wao sio al-Jamaa´ah. al-Jamaa´ah ni wale walio juu ya haki. Hawa ndio al-Jamaa´ah.

Ambaye anasema kuwa yeye anafuata kipote fulani na ndio al-Jamaa´ah. Nyinyi mnasema tulazimiane na al-Jamaa´ah na hawa ninaowafuata ndio al-Jamaa´ah. Tunawauliza nani kasema kuwa hawa ndio Jamaa´ah? al-Jamaa´ah ni wale walio katika haki na juu ya Sunnah. Hawa ndio al-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 19
  • Imechapishwa: 01/10/2017