07- Madhambi yanaudhoofisha mwili na moyo


Madhambi yanaudhoofisha moyo na mwili. Kuhusu kuudhoofisha moyo, ni jambo liko wazi. Bali yanaweza kuudhoofisha mpaka moyo ukafa kabisa kabisa.

Kuhusu kwamba yanaudhoofisha miwili, nguvu za muumini zinapatikana moyoni mwake. Kila ambavyo moyo wake unavokuwa na nguvu ndivyo mwili wake unakuwa na nguvu.

Kuhusu mtenda dhambi, basi yeye ndiye mdhaifu kabisa, japokuwa atakuwa ni mwenye nguvu kimwili. Katika hali hii nguvu zake zinakuwa ni zenye kumkhini pale anapozihitaji zaidi. Tafakari nguvu za kimwili za warumi na wafursi namna zilivyowakhaini pale walipozihitajia zaidi. Waumini waliwashinda kwa nguvu za kimwili na za nyoyo zao.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 28/01/2018