07. Baadhi ya alama za wazi za Ahl-us-Sunnah

Kuhusu Ahl-us-Sunnah, baadhi ya alama zao ni:

1- Wanalingania katika kukitendea kazi Kitabu cha Allaah (Ta´ala).

2- Wanaifasiri Qur-aan kwa Sunnah na mapokezi ya Maswahabah na Taabi´uun.

3- Wanalingania katika Sunnah Swahiyh zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

4- Wanaitakidi kuwa Sunnah ndio yenye kuibainisha na yenye kuifasiri Qur-aan.

5- Wanaipenda Sunnah, Ahl-us-Sunnah na wale wenye kuifikisha. Wanaonelea kuwa Allaah ameihifadhi dini kupitia wao. Ni fadhila kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) wanawapenda wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah. Abu Bakr bin ´Ayyaash aliulizwa ni nani Sunniy ambapo akajibu:

“Ambaye kunapotajwa matamanio hakasiriki kwa chochote katika hayo.”i

6- Wako kati na kati, kati ya upetukaji na uzembeaji.

7- Hawana msimamo wa ushabiki kwa yeyote katika maimamu wao mpaka wakaonelea kuwa wamekingwa na kukosea, pasi na kujali sawa wakiwa ni Maswahabah au wengineo.

8- Wanawachukia Ahl-ul-Bid´ah na wanamuabudu Allaah kwa kupambana nao na kuzibainisha Bid´ah zao ili watu watahadhari nao na watahadhari vilevile na Bid´ah zao.

9- Wanaitilia bidii ´Aqiydah na kuipa kipaumbele juu ya matendo mengine yote tofauti na wanavyofanya watu wa Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 10/02/2017