07. Allaah hashirikishwi na yeyote wala chochote


Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“… na wala asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!”

Mfano wake ni mtu kujionyesha au kutaka kusikika kwa ajili ya kitendo chake. Yule anayetenda kwa ajili ya kutaka kuonekana au kwa ajili ya kutaka kusikika basi Allaah anakibatilisha na kukivunjilia mbali kitendo chake. Amesema (Ta´ala):

أَحَدًا

“… yeyote… ”

Makatazo yametajwa kwa fomu isiyotambulika na hivyo inajumuisha kila kitu. Allaah hakubali ashirikishwe na yeyote, si katika Malaika, Mitume, mawalii, waja wema, mawe, miti, majini au watu. Hapa kuna Radd kwa wale wanaosema kwamba shirki ni kuyaabudu masanamu peke yake. Ama kujikurubisha na kufanya Tawassul kwa Allaah kupitia mawalii na waja wema hakuzingatiwi ni kama kuabudu masanamu. Hili ni batili. Kwani Allaah anasema:

وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“… na wala asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!”

Makatazo ni yenye kuenea na yanajumuisha kila anayeabudiwa badala ya Allaah; majini, watu, Malaika, Mitume, waja wema, mawalii na wengineo. Allaah hakubaliwi kushirikishwa katika ´ibaadah Yake yeyote au chochote kiwacho. Katika hilo hakuna tofauti kati ya masanamu, mawalii au makaburi. Yote hayo yanaingia ndani ya maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“… na wala asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 443
  • Imechapishwa: 02/09/2019