06. Namna Salaf walivokuwa wakikhofia shirki juu ya nafsi zao

Tambua kwamba shirki ni kitu kilichojificha mno. Aliiogopa Ibraahiym ambaye ndiye kiongozi wa kumpwekesha Allaah na kujiepushe na shirki. Allaah amesimulia juu yake:

وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ

“Uniepushe mimi na wanangu kuabudu masanamu.”[1]

Zingatia maneno Yake:

وَاجْنُبْنِي

“Niepushe mimi.”

Hakusema:

“Nizuie.”

Kwa sababu kuomba “kuepushwa” maana yake ni kwamba amweke upande wa ´ibaadah na masanamu ayaweke upande mwingine wa mbali. Hili ni lenye kuingia ndani zaidi kuliko “kuzuiwa”. Kwa sababu akiwa upande mmoja na shirki ikawa upande mwingine anakuwa mbali zaidi. Ibn Abiy Mulaykah amesema:

“Nilikutana na Maswahabah thelathini wa Mtume wa Allaah na kila mmoja anachelea unafiki juu ya nafsi yake.”[2]

Kiongozi wa waumini, ´Umar bin al-Khattwaab alisema kumwambia Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Nakuuliza kwa jina la Allaah! Je, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinitaja pamoja na wale aliowataja katika wanafiki?”

Licha ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbashiria Pepo lakini alichelea yasije hayo yakawa ni yale yaliyomdhihirikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na matendo yake kipindi cha uhai wake. Hakuna anayejiaminisha na unafiki isipokuwa tu ambaye ni mnafiki na hakuna anayekhofu unafiki isipokuwa tu muumini. Hivyo ni lazima kwa mja apambane na kumtakasia nia Allaah na apambane nafsi yake juu yake. Baadhi ya Salaf wamesema:

“Sijawahi kupambana na nafsi yangu juu ya chochote kama nilivyopambana nayo juu ya kumtakasia nia Allaah.”

Shirki jambo lake ni la khatari sana na si jambo jepesi. Allaah humfanyia wepesi mja akamtakasia nia. Hapo ni pale ambapo humfanya Allaah akawa mbele ya macho yake. Matokeo yake akawa ni mwenye kunuia kwa matendo yake uso wa Allaah.

[1] 14:35

[2] al-Bukhaariy (36).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 11
  • Imechapishwa: 17/06/2021