3- Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat. Maana yake ni kwamba tunamthibitishia Allaah yale majina na zile sifa alizojithibitishia nazo Mwenyewe au alizomthibitishia nazo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunafanya hivo pasi na kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna wala kuzifananisha. Inapaswa iwe kwa mujibu wa maneno ya Allaah (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

Tunamthibitishia Allaah majina kama alivosema Mwenyewe:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

”Allaah ana majina mazuri mno, hivyo basi muombeni kwayo na waacheni wale wenye kupondoka katika kuyapotosha majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.”[2]

Tunamsifu Allaah (´Azza wa Jall) kama alivyojisifia Mwenyewe; ya kwamba ni Mjuzi, Mwenye kurehemu, Mwenye kusikia, Mwenye kuona. Anasikia, anaona, anajua, anakasirika, anatoa, anazuia, anashusha, anapandisha. Zote hizi ni sifa za kimatendo.

Vilevile ana sifa za kidhati kama mfano wa uso, mikono na sifa nyenginezo za ukamilifu. Tunamthibitishia Allaah yale aliyojisifia Mwenyewe na yale aliyosifiwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ni mamoja katika sifa za kidhati na sifa za matendo.

[1] 42:11

[2] 07:180

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 07/08/2019