06. Malengo ya alama za Allaah


Akamjulisha juu ya alama za viumbe Wake – Ili ziweze kumjulisha uwezo wa Allaah (´Azza wa Jall). Anapozitazama mbingu, ardhi, nyota, milima, miti, bahari, ardhi, wanyama na vyenginevyo basi vinamjulisha juu ya uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye ndiye ambaye ameumba viumbe hivi vikubwa:

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

”Na katika alama Zake ni usiku na mchana, jua na mwezi. Hivyo basi msisujudie jua na wala mwezi, bali msujudieni Allaah ambaye aliyeviumba – ikiwa Yeye pekee ndiye mnamwabudu.”[1]

Alama za Allaah zimegawanyika katika sampuli mbili:

1- Alama za kilimwengu, nazo ni vile viumbe.

2- Alama za kiwahyi kukiwemo Qur-aan tukufu.

[1] 41:37

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 14
  • Imechapishwa: 30/06/2021