06. Kila kitu kimeshapangwa na kukadiriwa

[10] Ni wajibu kuamini Qadar, kheri na shari yake, matamu yake na machungu yake, makubwa yake na machache yake, yenye kuonekana na yenye kujificha, yale yenye kupendwa na yale yenye kuchukiwa na mazuri yake na yasiyokuwa mazuri.

Mwanzo na mwisho wake ni kutoka kwa Allaah. Amepanga mipango Yake juu ya waja Wake na akakadiria makadirio juu yao. Hakuna yeyote awezaye kushinda matakwa ya Allaah (´Azza wa Jall) na wala hakuna yeyote awezaye kushinda mipango Yake, bali wote hawana ujanja ni wenye kupita chini ya yale aliyowaumba kwayo. Huu ni uadilifu kutoka kwa Mola wetu (´Azza wa Jall). Anataka utiifu utendeka, yuko radhi nao, anaupenda na ameuamrisha. Hata hivyo hakuamrisha maasi na wala hayapendi na kuyaridhia. Upande mwingine ameyahukumu, akayakadiria na akataka yatendeke. Muuliwaji anauawa pindi muda wake unapofika.

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 31
  • Imechapishwa: 25/02/2019