Katika kipindi hichi hakukubaki kitu isipokuwa kuyadiriki yale yaliyopita, kuomba msamaha, kuomba du´aa, kufanya matendo mema ambayo mtu anaweza kwa sababu ya kuchunga wakati na kujiandaa kwa ajili ya safari.

Sarriy as-Saqatwiy alikuwa halali asipozidiwa na usingizi.

Kuna watu waliingia kwa al-Junayd alipokuwa amelala na kutaka kukata roho. Wanamkuta anafanya Rukuu´ na Sujuud. Akataka kukunja miguu yake katika swalah lakini hakuweza kufanya hivo kwa sababu roho ilikuwa imeanza kutoka kupitia miguu hiyo. Mtu mmoja akamuuliza kinachoendelea. Akasema:

“Hii ni neema ya Allaah kubwa.”[1]

´Aamir bin ´Abdi Qays alikuwa kila siku akiswali Rak´ah 1000 kwa siku. Mwanamme mmoja akakutana naye na kumwambia: “Nikwambie kitu?” Akajibu: “Ndio, ikiwa unaweza kusimamisha jua.”[2]

Mwanamme mwengine alimuuliza hali kadhalika. Akamwambia: “Fanya mbio, mimi nina haraka.” Ndipo mwanamume yule akasema: “Una haraka ya nini?” Akasema: “Roho yangu iko inataka kutoka.”[3]

´Uthmaan al-Baaqqilaaniy amesema:

“Nachukia kula chakula cha jioni mpaka wakati mwingine. Kula kunanishughulisha kutofanya Dhikr.”

Daawuud at-Twaa´iy alikuwa akila vipande vya biskuti badala ya kula mkate. Alipoulizwa juu ya hilo akasema:

“Muda wa baina ya kula mkate na vipande vya biskuti mtu anaweza kusoma Aayah 50.”

Kundi la watu liliingia kwa mtu mwema na kumwambia: “Huenda tunakushughulisha.” Akasema: “Mmesema kweli kabisa. Nilikuwa nasoma mkanizuia.”

Yule atakayetazama utukufu wa wakati basi atautumia. Imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesema “Subhaan Allaah wa bi Hamdih” basi hupandiwa mti wa mtende Peponi.”[4]

Tumewaona wazee wengi pindi wanapotembelewa na wageni wanapumzika na kusikiliza maneno yanayowadhuru na hayawanufaishi. Hakuna walichofanya isipokuwa kuupoteza tu muda wao. Lau wangelifahamu basi kufanya Tasbiyh ingelikuwa ni bora kwao. Yote haya hayatokani isipokuwa ni kwa sababu na kughafilika na Aakhirah. Kwa sababu Tasbiyh moja inafanya kupatikana thawabu tulizotaja ilihali maneno ya kidunia yanadhuru na wala hayanufaishi.

Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akifunga masiku pa joto kali. Alipoambiwa kuwa ni mzee, akajibu:

“Naiandaa kwa ajili ya siku ndefu.”

Kulisemwa kuambiwa mtu mwema awe na urafiki juu ya nafsi yake, akasema:

“Ni urafiki ndio ninaotafuta.”

Atayetambua utukufu wa wakati na thamani yake basi hatoutumia vibaya kwa muda wa kupepesa macho.

Mwache kijana aichunge bidhaa yake.

Mwache mtu wa wastani ajihifadhi kiasi na anavyoweza.

Mwache mzee ajizidishie akiba ili aweze kujiunga na kundi lake.

Mwache yule aliyefikia umri unyonge ajiandae na kufa wakati wowote.

[1] Hilyat-ul-Awliyaa’ (10/281).

[2] Hilyat-ul-Awliyaa’ (2/88-89).

[3] Swifat-us-Swafwah (3/210-211).

[4] Ibn Hibbaan (823),

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin al-Jawziy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyh-un-Naa’im al-Ghamr ´alaa Mawswim-il-´Umr, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 15/02/2017