06. Hakuna waislamu kwa mtazamo wa Sayyid Qutwub

Jambo la nne ni kwamba haizingatiwi kwamba ni Takfiyr kuelezea kwamba jamii ni ya kipindi cha kikafiri. Wala haiwatoi katika Uislamu. Wakati Abu Dharr aliposema kwa kumkejeli Bilaal kwamba ni mtoto wa cheusi, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

“Hakika wewe una chembechembe za kipindi cha kikafiri.”

Huko haikuwa kumkufurisha.

Ama kuhusu Sayyid Qutwub, inawezekana kweli alisema hivo kwa kukusudia kuikufurisha jamii. Kwa sababu jambo hilo linatambulika kwake[1].

[1] Sayyid Qutwub amesema:

”Walimwengu wamerudi katika kipindi cha kikafiri kama wakati ambapo ”hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” ilipokuja kwa watu. Walimwengu wameritadi na wameanza kuwaabudu viumbe na madhalimu wa kidini. Wameiacha ”hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” hata kama bado wapo waandishi wanakariri ”hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” kwenye minara pasi na kufahamu maana yake. Wote kwa jumla, wakiwemo wale kule juu katika minara ya ulimwenguni kote ambao wanakariri neno ”hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” pasi na kufahamu maana wala dalili zake… hawa wana dhambi kubwa zaidi na wanastahiki adhabu zaidi siku ya Qiyaamah. Kwa sababu wameritadi kwa kuwaabudu waja baada ya kwamba walikuwa ni wenye kuongoka na kuwa katika dini ya Allaah.” (Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (2/1057))

Amesema tena:

”Waislamu hawahitajii kupigana Jihaad hii leo kwa sababu hakuna waislamu. Suala wanalohitajia kulishughulikia ni la uwepo wa Uislamu na waislamu.”(Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (3/1634))

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 26/10/2018