06. Anayejiunga na makundi anakuwa mtu wa Bid´ah?


Swali 6: Je, yule mwenye kujiunga na makundi anazingatiwa kuwa ni mtu wa Bid´ah?

Jibu: Hili inategemea na makundi yenyewe. Yule mwenye kujiunga na makundi yanayoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah ni mtu wa Bid´ah[1].

[1] Shaykh Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd amesema:

“Hakuna yeyote katika Ummah wetu mbali na Nabii na Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anayetakiwa kufanywa ni mtu ambaye ni lazima kufuatwa na kupenda na kuchukia kwa ajili yake. Yule mwenye kuteua mtu kama huyo ni mpotevu mtu wa Bid´ah.” (Hukm-ul-Intimaa’ ilaa al-Firaq wal-Ahzaab wal-Jamaa´aat al-Islaamiyyah, uk. 96-97)

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakuna mtu yeyote mwenye kuteuliwa katika Ummah mbali na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo kunaitwa katika madhehebu yake na kupenda na kuchukia kwa ajili yake. Hakuna yeyote ateuae maneno mbali na Maneno ya Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maafikiano ya Ummah ambayo kunapendwa na kuchukia kwa ajili yake. Haya ni mambo ya Ahl-ul-Bid´ah ambao huteua mtu au maneno yanayoutenganisha Ummah kwayo. Wanapenda na kuchukia kutokana na maneno au mtu huyo.” (Majmuu ´-ul-Fataawaa (20/164))

Shaykh Bakr amesema baada ya maneno ya Shaykh-ul-Islaam yaliyoko juu:

“Hii ndio hali ya makundi na mapote mengi ya Kiislamu hii leo. Huwateua watu kama viongozi wao. Wanawapenda watu walio pamoja nao na wanawachukia walio dhidi yao. Wanawatii kwa kila wanachokisema pasina kurejea katika Qur-aan na Sunnah na bila kuwauliza dalili kwa yale wanayoyasema au kuyafanya.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 18/02/2017