06. al-Ismaa´iyliy anabainisha ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah kuhusu sifa


18- Abul-´Abbaas Mas´uud bin ´Abdil-Waahid bin Matwar al-Haashimiy ametukhabarisha: Haafidhw Abul-´Alaa’ Swaa´id bin Sayyaar al-Harawiy  ametuhadithia: Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad al-Jurjaaniy ametuhadithia: Abul-Qaasim Hamzah bin Yuusuf as-Sahmiy ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin Ibraahiym al-Ismaa´iyliy ametuhadithia na kusema:

“Tambueni – Allaah aturehemuni sisi na nyinyi – ya kwamba madhehebu ya Ahl-ul-Hadiyth, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake na kukubali yale yaliyomo katika Kitabu cha Allaah (Ta´ala) na mapokezi Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hayatakiwi kuachwa wala kurudihswa. Wameamrishwa kufuata Qur-aan na Sunnah na wanaonelea kuwa vyote viwili vina uongofu. Wanashuhudia ya kwamba Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwenye kuongoza katika njia iliyonyooka na ni wenye hadhari wasije kupatwa na fitina na adhabu yenye kuumiza kwa sababu ya kwenda kinyume naye.

Wanaamini kuwa Allaah (Ta´ala) ni mwenye kuitwa kwa majina Yake mazuri aliyojiita Mwenyewe, ni mwenye kusifiwa kwa sifa Zake nzuri alizojisifu Mwenyewe na akamsifu kwazo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Amemuumba Aadam kwa mkono Wake.

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

“Bali mikono Yake imefumbuliwa hutoa atakavyo.”[1]

Haitakiwi kwa mtu kuifanyia namna.

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ‘Arshi.”[2]

Haitakiwi vilevile kwa mtu kuifanyia namna. Ameweka wazi ya kwamba amelingana juu ya ´Arshi na wala Hakutaja amelingana vipi.”[3]

[1] 05:64

[2] 10:03

[3] I´tiqaadu A’immati Ahl-il-Hadiyth, uk. 396

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta'wiyl, uk. 15
  • Imechapishwa: 02/05/2018