06. Du´aa wakati wa kumwingilia mke


4- Anayotakiwa kusema wakati wa kumwingilia

Anatakiwa kusema yafuatayo wakati anapomwingilia mke wake:

بسم الله اللهم جنبنا الشيطان وجنب الشيطان ما رزقتنا

“Naanza kwa jina la Allaah! Ee nilinde na shaytwaan na Kilinde na shaytwaan kile utachoturuzuku.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na hili:

“Endapo Allaah amewaandikia kupata mtoto basi kamwe shaytwana hatomdhuru.”[1]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake (09/187) na waandishi wengine wa “as-Sunan” isipokuwa an-Nasaa´iy, katika “al-´Asharah” (01/79), ´Abdur-Razzaaq (06/193), at-Twabaraaniy (02/151/3) kupitia kwa Anas. Vilevile imepokelewa katika “al-Irwaa´-ul-Ghaliyl” (2012) kwa ukamilifu zaidi kuliko hapa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 98
  • Imechapishwa: 23/02/2018