Jina likiwa ni lenye kulazimiana na Allaah (لازماً ) basi Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanamthibitishia Allaah jina hilo, wanamwita na wanamuomba Allaah kwalo. Vilevile wanathibitisha ile sifa inayofahamishwa na jina hilo kwa njia kamilifu zaidi inayolingana na Allaah (Ta´ala). Lakini hapa hakuna athari yoyote. Kwa sababu jina hili limenyofolewa kutoka katika kitu kisichopelekea katika sifa nyingine juu ya yule mwenye kusifiwa. Kwa ajili hiyo ndio maana halina athari.

Tupige mfano wa jina la Aliye hai (الحي). Hili ni miongoni mwa majina ya Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo tunamthibitishia jina hili Allaah na tunasema kuwa Aliye hai ni miongoni mwa majina ya Allaah (Ta´ala). Tunamuomba kwalo kwa kusema “Ee Uliye hai na msimamizi wa kila kitu.” Tunaamini ile sifa inayofahamishwa nalo. Ni mamoja sifa hiyo ni yenye kulazimiana na Allaah au sio yenye kulazimiana na Allaah. Inahusiana na uhai mkamilifu ambao ndani yake umekusanya sifa zote kamilifu kwa aliye hai kama vile elimu, uwezo, usikizi, uoni, kuzungumza na nyenginezo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 12-13
  • Imechapishwa: 30/06/2019