05. Mazazi sio katika dini ya Uislamu

Kwa hiyo inamdhihirikia kila ambaye ana utambuzi japo kidogo, anataka haki na inswafu  katika kuitafuta ya kwamba kusherehekea mazazi sio katika dini ya Uislamu. Bali ni miongoni mwa Bid´ah zilizozuliwa ambazo zimeamrishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuziacha na kutadharisha nazo. Haitakikani kwa mwenye busara kudanganyika na wingi wa watu wanayoyafanya katika nchi nyingi. Kwani hakika haki haitambuliki kwa wingi wanaoifanya. Haki inatambulika kwa dalili za ki-Shari´ah. Amesema (Ta´ala) juu ya mayahudi na manaswara:

قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

“Sema: “Leteni ushahidi wenu mkiwa ni wakweli.”[1]

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ

“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, basi watakupoteza na njia ya Allaah.”[2]

[1] 02:111

[2] 06:116

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 10
  • Imechapishwa: 12/01/2022