Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah kwa kumpwekesha, kunyenyekea Kwake kwa utiifu na kujitenga mbali na shirki na washirikina. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

”Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.” (03:19)

وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

”Na Nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.” (05:03)

وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

“Na rejeeni kwa Mola wenu na jisalimisheni Kwake kabla haijakufikieni adhabu kisha hamtonusuriwa. ” (39:54)

فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

“Basi msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.” (02:132)

وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

”Msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.” (03:102)

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ

Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi – akipenda asipende – na Kwake watarejeshwa.” (03:83)

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote atakayefanya dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (03:85)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
  • Imechapishwa: 05/08/2020