04. Lulu kuhusu ´Aliy bin Hamshaad


4- ´Aliy bin Hamshaad (kfrk. 338) tabaka 11

adh-Dhahabiy ameandika wasifu wake katika “at-Tadhkirat-ul-Huffaadhw” na akasema:

“Haafidhw mkubwa Abul-Hasan an-Naysaabuuriy, mtunzi wa tungo nyingi. Alisikia kutoka kwa al-Husayn bin al-Fadhwl, al-Fadhwl ash-Sha´raaniy, al-Haarith bin Abiy Usaamah, Ibraahiym bin Dayziyl, Ismaa-iyl al-Qaadhwiy na wengineo.

al-Haakim amesikia kutoka kwake, akamsifu na akamuadhimisha kwa hali ya juu. Kitabu chake “al-Musnad” kina juzu 400, “al-Ahkaam” yake ina juzu 260 na tafsiri yake ya Qur-aan ina mijeledi kumi.

Abu Ahmad al-Haakim amepokea kutoka kwake na akasema:

“Sijawahi kumuona yeyote katika wanachuoni wetu ambaye ni thabiti zaidi kama yeye.”

Mtoto wake amesema:

“Sijui kama kuna siku yoyote baba yangu aliacha swalah ya usiku.”

Alifariki katika Shawwaal mwaka wa 338. Allaah amrehemu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tadhkiyr-un-Naabihiyn, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 10/06/2019