686- Abu Sa´iyd ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Atakayefanya matendo matano kwa siku basi Allaah humwandika ni katika watu wa Peponi: atakayemtembelea mgonjwa, akashuhudia jeneza, akafunga, akaenda swalah ya ijumaa na akaachia mtumwa huru.”

Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/431)
  • Imechapishwa: 27/01/2017