03. Sifa ya pili nzuri kwa mfungaji


2- Malaika humuombea msamaha mpaka akate swawm. Malaika ni waja wenye kukirimiwa mbele ya Allaah:

لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

”Hawamuasi Allaah kwa yale anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[1]

Wako karibu zaidi na kukubaliwa du´aa yao na Allaah juu ya wafungaji kwa vile amewaidhinisha kufanya hivo. Allaah amewaidhinisha kuwaombea msamaha wafungaji wa Ummah huu kwa kukuza shani yao, kunyanyua utajo wao na kubainisha ubora wa funga zao. Kuombewa msamaha ni kusitiriwa madhambi duniani na Aakhirah na kuyapuuza. Ni miongoni mwa makusudio na malengo makuu kabisa. Kila mwanadamu ni mwingi wa kukosea na wenye kupindukia mipaka juu ya nafsi yake na hivyo ni mwenye kulazimika kumuomba msamaha Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 66:06

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 25/03/2020