03. Nguzo za subira


Wanachuoni wamesema pia kwamba subira juu ya makadirio ya Allaah yenye kuumiza yamegawanyika aina tatu:

1- Kuizuia nafsi juu ya kutokata tamaa.

2- Kuuzuia ulimi kutomlalamikia mwengine asiyekuwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala).

3- Kuzuia viungo vya mwili kutopiga mashavu na kuchana nguo.

Kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mafungano ya subira juu ya dini ni kama kichwa juu ya kiwiliwili. Hana imani yule ambaye hana subira.”[1]

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Nimepata kwamba Allaah ametaja subira ndani ya Qur-aan mara tisini.”

Hii ni dalili inayoonyesha umuhimu na nafasi ya subira. Subira ina nafasi kubwa katika dini. Ni lazima kwa muumini awe na subira juu ya yale matatizo, mazito na majanga anayokutana nayo katika maisha haya. Afanye subira kwa ajili ya kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] ´Abdur-Razzaaq (21031), Ibn Abiy Shaybah (6/172) na al-Bayhaqiy katika ”Shu´ab-ul-Iymaan” (7/124).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 431
  • Imechapishwa: 13/08/2019