02. Uislamu na Sunnah ni vitu viwili vilivyolazimiana


Hakuna tofauti kati ya hivyo viwili. Tukifasiri Sunnah kuwa ni njia, kutakuwa hakuna tofauti kati yake na Uislamu.

Uislamu hausimami isipokuwa kwa Sunnah kama jinsi Sunnah haiwezi kusimama isipokuwa kwa Uislamu. Yule ambaye anadai Uislamu na wala hatendei kazi Sunnah – bi maana njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – sio Muislamu. Vilevile yule anayejua Sunnah na wala hajisalimishi kwa Allaah, sio Muislamu hata kama ataijua Sunnah. Hivyo ni lazima kukusanya kati ya vyote viwili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 14
  • Imechapishwa: 13/06/2017