1- Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا

”Anayetaka maisha ya dunia… “

Bi manaa yule ambaye kwa atafanya kitendo cha kidini kwa ajili ya kutaka jambo la kidunia.

وَزِينَتَهَا

“… na mapambo yake… “

Bi maana mali na watoto. Amesema (Ta´ala):

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا

“Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia.”[1]

Maneno Yake (Ta´ala):

 نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا

“… basi Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa humo…

Haya ndio malipo. Ikiwa Allaah anataka basi humpa katika dunia alichokusudia na alichotaka ili baadaye amuadhibu na atangamane nae kwa mujibu wa nia yake. Amesema (Ta´ala):

مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا

“Yeyote anayetaka [starehe za dunia] ipitayo upesi, basi Tunamharakizia humo tuyatakayo na kwa tumtakaye – halafu tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa ni mwenye kutwezwa na ni mwenye kufukuziliwa mbali.”[2]

Maneno Yake (Ta´ala):

وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ

“… nao hawatopunjwa humo… “

Hakutopunguzwa chochote. Maneno Yake (Ta´ala):

أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الآخِرَةِ إِلاَّ النَّارُ

“… [lakini] hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto.”

Hapa kumebainishwa adhabu yao. Watapata katika yale mambo ya kidunia yale waliyotaka na waliyotafuta, lakini Aakhirah hawana thawabu zozote. Kwa sababu hawakutaka Aakhirah. Thawabu za Aakhirah anapewa yule mwenye kuzitaka:

وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا

“Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia bidii ipasavyo, ilihali ni muumini, basi hao bidii zao ni za kushukuriwa.”[3]

Maneno Yake (Ta´ala):

وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا

“Yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani]… “

Ni yenye kuharibika huko Aakhirah yale waliyofanya hapa duniani. Maneno Yake (Ta´ala):

وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

“… na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”

Ubatilikaji unakuwa hapa duniani na ukhasirikaji unakuwa huko Aakhirah. Matendo yao ni yenye kubatilika hapa duniani kwa sababu hayakufanywa kwa ajili ya Allaah. Kwa hiyo Aakhirah matendo yao ni yenye kubatilika.

[1] 18:46

[2] 17:18

[3] 17:19

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 448-449
  • Imechapishwa: 03/09/2019