02. Mwenye ´Aqiydah mbovu yumo khatarini


Mtu kuwa na kasoro katika ´Aqiydah, ikiwa kasoro hiyo inaivunja, basi mtu hasamehewi. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.” (04:48)

Kuhusu madhambi yaliyo chini ya shirki, japokuwa yatakuwa ni makubwa, bado kuna matumaini Allaah akayasamehe:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.” (04:48)

Bi maana madhambi yaliyo chini ya shirki anamsamehe amtakaye. Hii ni dalili ya kuwa ´Aqiydah ndio asili na ndio msingi, nayo ndio ambayo ni wajibu kwa mtu ajifunze nayo kama ilivyokuja katika Qur-aan, Sunnah na walivyoichukua na kuifuata Salaf wa Ummah huu. Kwa kuwa ikiwa ni mjinga na haijui ´Aqiydah, basi anaweza kutumbukia katika mambo yanayokwenda kinyume nayo. Hili khaswa khaswa watu wengi wanayafanya mambo yanayoitia dosari ´Aqiydah. Mambo hayo yanaweza kuiharibu na kuibatilisha kabisa kama ambavyo vilevile yanaweza kuipunguza. Ikiwa mtu hajui ´Aqiydah sahihi wala hakujifunza nayo, basi anaweza kuiharibu ´Aqiydah yake na wakati huohuo hajui. Kwa kuigiza mambo wayafanyayo baadhi ya watu au kwa sababu ya kuwafuata walinganizi wapotofu ambao wanawaita watu katika kuziharibu ´Aqiydah zao. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

“Allaah ni mlinzi wa wale ambao wameamini; Anawatoa kutoka katika viza na  kuwaingiza katika nuru.  Na wale ambao wamekufuru walinzi  wao ni Twaaghuut; huwatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa Motoni wao humo watadumu milele.” (02:257)

Huwatoa katika nuru – yaani katika ´Aqiydah sahihi na uwongofu – na wanawaingiza katika viza – bi maana katika shirki, Bid´ah, mambo uzushi na ukhurafi. Hivi ndivo viza. Katika haya kuna tahadhari kwa muislamu akaja kuiharibu ´Aqiydah yake naye hajui au akawaamini walinganizi wapotofu. Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam):

“Kikubwa ninachokhofia juu ya Ummah wangu ni viongozi wapotofu.”

Na ni wingi ulioje hii leo! Allaah asiwafanye kuwa wengi. Kuanzia hapa, tunabainikiwa ya kwamba ni wajibu kwa muislamu kuitilia umuhimu na kuichunga ´Aqiydah yake na ajifunze nayo kutoka katika vyanzo vyake sahihi. Himdi zote anastahiki Allaah kumeandikwa vitabu vikubwa na vifupi vinavyoisherehesha na kuibainisha ´Aqiydah na vilevile vinabainisha yanayoiweka madoa na kuiharibu. Vimeenea.

Ni lazima kwa muislamu kusoma vitabu hivi vyenye faida kuhusu maudhui ya ´Aqiydah mpaka awe na msimamo juu yake na ajiepushe na yanayopingana nayo na kuiharabu. Jambo hili sio sahali. Jambo hili ni muhimu sana.

Yapo mambo mengi yanayofanywa na watu wengi. Huenda wakajiita kuwa ni waislamu na wakajidai kuwa na elimu pia. Watu hawa wanayafanya mambo yanayopingana na ´Aqiydah:

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah al-Islaamiyyah as-Swahiyhah https://www.youtube.com/watch?v=KqoTCYds6Cs&t=13s
  • Imechapishwa: 22/07/2018