02. Misingi misita iliyobainishwa na Allaah


Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Miongoni mwa ajabu ya maajabu na alama kubwa zenye kufahahamisha uwezo wa Mfalme mwenye kushinda ni misingi sita ambayo Allaah (Ta´ala) ameibainisha ubainifu wa wazi [kuwabainishia] watu wa kawaida wasiokuwa na elimu zaidi ya vile wanavyodhania wenye kudhania. Halafu baada ya haya wakakosea walimwengu wengi werevu na wenye akili isipokuwa wachache katika wachache.

MAELEZO

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) hutilia umuhimu vijitabu vifupivifupi ambavyo wanavifahamu watu wa kawaida na wanafunzi. Miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu hiki ”Sittati Usuwl ´Adhwiym”. Nayo ni ifuatayo:

1- Msigni wa kwanza: Kumtakasia Allaah nia na ubainifu wa kinyume chake ambacho ni shirki.

2- Msingi wa pili: Kukusanyika katika dini na makatazo ya kufarikiana humo.

3- Msingi wa tatu: Kuwasikiliza na kuwatii watawala.

4- Msingi wa nne: Ubainifu wa elimu na wanachuoni, Fiqh na Fuqahaa´ na wale wenye kujifananisha nao ilihali si katika wao.

5- Msingi wa tano: Ubainifu ni kina nani mawalii.

6- Msingi wa sita: Kurudi hoja tata zilizowekwa na shaytwaan katika kurudisha nyuma Qur-aan na Sunnah.

Misingi hii ni muhimu na inayostahiki kutiliwa umuhimu. Na sisi tunamwomba Allaah msaada katika kuifafanua na kuiwekea taaliki kwa yale ambayo Allaah atasahilisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 05-07
  • Imechapishwa: 15/06/2021