02. Kinga ya pili ya janga la corona: Kusoma kwa wingi du´aa ya Yuunus

2- Kusema kwa wingi du´aa ya Yuunus

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ

“Dhan-Nuun alipoondoka akiwa ameghadhibika akadhani kuwa hatutamdhikisha akaita katika kiza kwamba: “Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu. Hivyo Tukamuitikia na tukamuokoa kutokamana na dhiki – na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo waumini.”[1]

Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hivo ndivo tunavyowaokoa waumini pindi wanapokuwa kwenye shida na wakatuomba hali ya kuwa ni wenye kutubia Kwetu, na khaswa wakiomba kwa du´aa hii katika hali ya matatizo.”[2]

Kisha akataja Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Du´aa ya Dhun-Nuun aliyoomba akiwa tumboni mwa nyangumi:

لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”

Hakuna muislamu yeyote aliyeomba hivo isipokuwa Allaah humwitikia.”[3]

´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakujapatapo kuondoshwa shida yoyote ya kidunia kama kumwabudu Allaah peke yake. Ndio maana du´aa katika mnasaba wa matatizo iliyoambatana na Tawhiyd, du´aa ya Dhun-Nuun ambayo hakuna yeyote mwenye matatizo aliiomba isipokuwa Allaah humwondolea matatizo yake kwa Tawhiyd. Hakuna chochote kinachopelekea kwenye matatizo makubwa isipokuwa shirki kama ambavo hakuna kinachosalimisha kutoka humo isipokuwa Tawhiyd. Tawhiyd ndio kimbilio, ulinzi na msaada wa viumbe wote.”[4]

[1] 21:87-88

[2] Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhiym (3/257).

[3] Ahmad na at-Tirmidhiy.

[4] al-Fawaa-id, uk. 86-87

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 5-7
  • Imechapishwa: 30/03/2020