02. Hadiyth “Yule mwenye kusimama Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio… “


993- Kutoka kwake (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza vilevile:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa alikokoteza juu ya kusimama nyusiku za Ramadhaan bila ya kuwalazimisha. Kisha akasema: “Yule mwenye kusimama Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/582-583)
  • Imechapishwa: 12/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy