02. Hadiyth “Allaah ampambe mtu ambaye amesikia mazungumzo kutoka kwetu… “

90- Zayd bin Thaabit ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ampambe mtu ambaye amesikia mazungumzo kutoka kwetu ambapo akawafikishia wengine. Huenda ambaye amebeba uelewa akamfikishia ambaye ana uelewa zaidi kuliko yeye. Huenda ambaye amebeba uelewa yeye mwenyewe sio mwelewa.

Moyo wa muislamu hauyaonei wivu kwa mambo: kumtakasia kitendo cha Allaah, kumnasihi mtawala na kulazimiana na mkusanyiko. Kwa sababu kuwaombea du´aa wao kunawazunguka walio nyuma yake wote.

Yule ambaye dunia ndio hamu yake kubwa, basi Allaah atamsabaratishia jambo lake, ataweka ufakiri mbele ya macho yake na hatopata katika dunia isipokuwa kile alichoandikiwa. Na yuile ambaye Aakhirah ndio malengo yake, basi Allaah atamkusanyia jambo lake, ataweka utajiri ndani ya moyo wake na dunia itamjilia hali ya kuwa si mwenye kuijali.”[1]

Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake na al-Bayhaqiy. Sehemu ya mwanzo ya Hadiyth mpaka katika maneno yake “… yeye mwenyewe sio mwelewa.” Imepokelewa na Abu Daawuud, at-Tirmidhiy ambaye ameifanya kuwa nzuri, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah kwa ziada ambayo inakosekana kwa hao wote wawili.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/147-148)
  • Imechapishwa: 01/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy