02. Filamu na Anaashiyd kwenye vituo vya majira ya joto


Swali 2: Kwenye majira ya joto kunachezwa filamu na Anaashiyd. Ni yapi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Ni wajibu kwa wasimamizi wa vituo vya majira ya joto kusitisha vitu vyote visivyokuwa na faida au vyenye madhara kwa wanafunzi. Wawafunze Qur-aan, Sunnah, Hadiyth, Fiqh na lugha ya kiarabu. Yanatosheleza na kwa kule kuchukua wakati. Wanatakiwa kuwafunza pia elimu ambayo itakuja kuwanufaisha katika dunia kama mfano wa kuandika, hesabu na ujuzi wenye faida. Mambo yanayoitwa “burudani” hayatakiwi kuwepo kwenye barnamiji[1]. Yanapoteza wakati. Pengine hata yakawasumbua na lile lengo lililowaleta. Miongoni mwa mambo hayo ni filamu na Anaashiyd. Haya si jengine isipokuwa ni pumbazo na mchezo. Ukiongezea juu ya hilo yanawafanya wanafunzi kuangalia michezo ya kuigiza na kusikiliza muziki unaorushwa kwenye vyombo vya khabari.

[1] Shaykh Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kitu ambacho inatakikana kukisisitiza ni yale ambayo vijana wengi wenye dini wametumbukia ndani yake. Wanasikiliza Anaashiyd zinazoimbwa kwa sauti za pamoja na wanaziita kuwa ni “Anaashiyd za Kiislamu”. Ni aina ya nyimbo na wakati mwingine zinaimbwa kwa sauti zenye kufitinisha. Mikanda hii inauzwa pamoja na mikanda ya Qur-aan na mihadhara ya dini. Anaashiyd hizi kuziita kuwa ni “Anaashiyd za dini” ni makosa. Kwa sababu Uislamu haukutuwekea Anaashiyd. Kinyume chake umetuwekea kumdhukuru Allaah, kusoma Qur-aan, kujifunza elimu yenye manufaa na kadhalika.

Kuhusiana na Anaashiyd ni katika dini ya Suufiyyah iliyozushwa. Wameifanya dini kuwa ni pumbazo na mchezo. Kuzifanya Anaashiyd ni katika dini ni jambo limeshabihiana na manaswara ambao dini yao wameifanya nyimbo na sauti za pamoja.

Lililo la wajibu ni kutahadhari na Anaashiyd hizi na kupiga marufuku kuuzwa na kusambazwa. Isitoshe Anaashiyd hizi zinaweza kuchochea katika hamasa zenye fitina na uchochezi kati ya waislamu.

Wanaeneza Anaashiyd hizi kwa kutumia hoja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaweza kusomewa mashairi na akasikiliza na kuzikubali. Jibu ya hilo ni kwamba mashairi yaliyokuwa yakisomwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayakuwa yanasomwa kwa sauti za pamoja kwa sampuli ya nyimbo. Vilevile hayakuwa yanaitwa “ya Kiislamu”. Ilikuwa ni mashairi ya kiarabu yaliyo ndani yake na hekima, methali, ujasiri na ukarimu. Maswahabah walikuwa kila mmoja akiyasoma kivyake kutokana na maana yaliyokuwa nayo. Walikuwa wanaweza kusoma mashairi wakati wanapofanya kazi za nguvu kama ya ujenzi au safari za usiku. Ni dalili inayoonyesha kuwa yameruhusiwa mambo kama hayo katika hali kama hizo, sio kuyafanya kuwa ni somo katika kulea na kufanya Da´wah, kama inavyofanya leo pindi wanafunzi wanapojifunza Anaashiyd hizi na kuziita kuwa ni “Anaashiyd za Kiislamu” au “Anaashiyd za kidini”. Hii ni Bid´ah katika dini na zinatoka katika dini ya Suufiyyah iliyozushwa. Wao ndio wenye kujulikana kufanya Anaashiyd kuwa ni kipengele cha dini.

Ni wajibu kuzindua kampeni hizi na kupiga marufuku kuuzwa mikanda hii. Shari huanza ikiwa ndogo. Ikiwa mtu hazisimamishi mapema zitakuja kuendelea na kukua.” (al-Khutab al-Minbariyyah (03/184-185)

Muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn aliulizwa kuhusu Anaashiyd za Kiislamu. Hapa chini kunafuatia swali na jibu:

Swali: Je, inajuzu kwa wanaume kuimba Anaashiyd za Kiislamu? Je, inajuzu kuwapigia dugu wanapoimba? Je, inajuzu kuimba Anaashiyd mbali na sikukuu na sherehe?

Jibu: Anaashiyd za Kiislamu ni Anaashiyd zilizozushwa. Zimeshabihiana na waliyozusha Suufiyyah. Kwa hivyo inatakiwa kwa mtu kujitenga nazo mbali kwa mawaidha katika Qur-aan na Sunnah. Isipokuwa tu labda katika vita ili ziweze kusaidia kuleta motisha na Jihaad katika njia ya Allaah (Ta´ala). Ni vizuri. Anaashiyd zikifuatanishiwa na dufu zinakuwa bado ziko mbali kabisa na usawa. (Fataawaa ash-Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (01/134-135))

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 20-22
  • Imechapishwa: 08/10/2016