02. Ahl-us-Sunnah wamejinasibisha na Sunnah za Mtume tofauti na Ahl-ul-Bid´ah wengineo


Ahl-us-Sunnah – Sunnah ni njia aliokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maneno yake, matendo yake na yale aliyoyakubali. Wameitwa Ahl-us-Sunnah kwa sababu ya kujinasibisha kwao na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na maneno na madhehebu mengineyo tofauti na wanavofanya Ahl-ul-Bid´ah ambao wanajinasibisha katika Bid´ah na upotevu wao. Kama mfano wa Qadariyyah na Murji-ah. Wakati mwingine wanajinasibisha na yule kiongozi wao. Kama mfano wa Jahmiyyah. Wakati mwingine wanajinasibisha na matendo yao mabaya. Kama mfano wa Raafidhwah na Khawaarij.

Wal-Jamaa´ah – Mkusanyiko maana yake ya kilugha ni kundi la watu lililokusanyika. Makusudio hapa ni wale waliokusanyika juu ya haki iliothibiti katika Qur-aan na Sunnah. Nao si wengine ni Maswahabah na wale wenye kuwafuata kwa wema japokuwa watakuwa wachache. Hivyo ndivyo alivyosema Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh):

“al-Jamaa´ah (mkusanyiko) ni yale yenye kufikiana na haki hata kama mtu atakuwa mmoja. Wakati huo hapo wewe utakuwa ni mkusanyiko.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 06
  • Imechapishwa: 07/02/2018