01. Yule mwenye kuvielewa vitabu tu       

Elimu inaweza kutafutwa kwa njia mbili:

1- Kukaa na kuwasikiliza wanachuoni.

2- Kusoma vitabu.

Upande mwingine njia ya kwanza ndio yenye kufungua njia ya pili. Upande mwingine uhakika wa njia ya pili imejengwa juu ya njia ya kwanza. Baadhi ya wanachuoni wamesema:

“Kwanza elimu ilikuwa kwenye vifua vya wanaume. Kisha ndio ikaanguka katika vitabu, lakini funguo zake ziko kwenye mikono ya wanaume.”

Vitabu ni muhimu katika maisha ya mwanafunzi, lakini yule tu ambaye amesoma chini ya wanachuoni na kufahamu maana ya maneno yao ndiye awezae kuelewa vitabu na namna ya kutangamana navyo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Twaalib-ul-´Ilm wal-Kutub
  • Imechapishwa: 03/05/2020