01. Utangulizi wa kitabu ”Fadhwaa-il-ush-Shaam”

Allaah (Ta´ala) ameufanya mji mtukufu wa Makkah ndio uanzilishi wa viumbe na amri Yake. Kitu cha kwanza alichoumba Allaah katika ardhi ilikuwa ni sehemu ya Ka´bah. Kuanzia hapo ndipo ardhi ilipanuka. Hapo ndipo kulipojengwa msikiti wa kwanza ulimwenguni juu ya kumuabudu Allaah peke yake. Hapo ndipo kulipoanza ujumbe wa Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kukateremshwa Kitabu chenye kubainisha.

Allaah (Ta´ala) ameifanya Shaam kuwa ndio mwisho wa viumbe na amri. Katika zama za mwisho imani na waumini watatulia Shaam. Shaam ndio mahali pa Mkusanyiko na watu watafufuliwa kutokea hapo.

Nimekusanya katika kitabu hichi yaliyopokelewa kuhusu kwamba Shaam italindwa na kuhifadhiwa kutokana na ile imani na Uislamu uliyomo. Nimefanya hivo ili kuzifanya vizuri nyoyo za watu wa Shaam na ili waweze kuhisi utulivu kutokana na yale majanga yaliyowakumbuka watu wa Shaam katika mwaka wa 721-722.

Ninamuomba Allaah atupe sisi na waislamu mwisho mwema na atufanye kuwa miongoni mwa kundi lilisimama kwa haki na shindi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 27
  • Imechapishwa: 02/02/2017