01. Misingi inayotofautisha kati ya muislamu na mshirikina

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake. Ama baada ya hayo;

Hii ni al-Qawaa´id al-Arba´ah ambayo mtunzi (Rahimahu Allaah)  ameifanyia uzindushi. Ni misingi ambayo ni muhimu. Mwenye kuielewa na kuifahamu vizuri, basi ataifahamu dini ya washirikina na dini ya waislamu. Viumbe wengi hawaifahamu misingi hii na ndio maana mambo yamewatatiza. Matokeo yake wakayaabudia makaburi, waliyomo ndani , mawalii, miti na mawe badala ya Allaah na huku wakihesabu kuwa wako juu ya kitu. Hilo ni kutokana na ujinga wa kutojua uhakika wa Tawhiyd na shirki.

Mtunzi wa misingi hii ni Shaykh na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Mi msafishaji ambaye aliusafisha ulimwengu wa Kiislamu katika bara hili katikati ya karne ya kumi na mbili. Alifariki 1206 H.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 7
  • Imechapishwa: 23/03/2023