1079- Abu Hurayrah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyeacha maneno ya uongo, kuyatendea kazi na ujinga, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na katika upokezi wa Ibn Maajah imekuja:

“…. Yule asiyeacha maneno, ujinga na kuutendea kazi.”[2]

Ni moja katika mapokezi ya an-Nasaa´iy pia.

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/624)
  • Imechapishwa: 24/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy