01. Hadiyth “Ukimwambia rafiki yako siku ya ijumaa nyamaza… “


716- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Ukimwambia rafiki yako siku ya ijumaa nyamaza ilihali huku imamu yuko anatoa Khutbah, basi umefanya upuuzi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah.

Upuuzi imesemekana kuwa maana yake ni kupoteza ujira. Maoni mengine yanasema umezungumza. Maoni mengine yanasema kuwa umefanya kosa. Maoni mengine yanasema kuwa swalah yako ya ijumaa imebatilika. Maoni mengine yamesema swalah yako ya ijumaa inageuka kuwa Dhuhr. Vilevile kuna maoni mengine yasiyokuwa hayo[2].

[1] Swahiyh.

[2] Haya maoni ya mwisho, na pia yaliyo kabla yake, ndiyo tunayoegemea. Kwa sababu kitu bora kinachoweza kuyafasiri ni maneno yake mwenyewe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Yule mwenye kufanya upuuzi na akajipenyeza kati ya watu basi anakuwa na Dhuhr.”

Maoni haya ndio anayoonelea Ibn Khuzaymah kwa kukata katika “as-Swahiyh” yake (03/155). Wala hili halipingani na maneno ya Ubayy:

“Huna katika swalah yako isipokuwa kile ulichofanya upuuzi.”

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsapoti kwa kusema:

“Amesema kweli Ubayy.”

Katika hali hii ni ile fadhilah ya swalah ya ijumaa ndio yenye kuondoshwa, na sio ijumaa yenyewe. Ni kama mfano wa kusema:

“Hakuna mvulana isipokuwa ´Aliy.”

 Hilo halilazimishi kuondoshwa kwa fadhilah kutoka katika msingi wake, isipokuwa sehemu yake. Fadhilah zilizobaki zinalingana na fadhilah za Dhuhr. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kufanya upuuzi na akajipenyeza kati ya watu basi anakuwa na Dhuhr.”

Alisema hivo kumwambia yule aliyefanya upuuzi au kujipenyeza kati ya watu. Yule mwenye kufanya upuuzi peke yake basi ana haki zaidi ya kuguswa na Hadiyth. Hilo ndio la dhahiri na liko wazi na himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/447)
  • Imechapishwa: 14/01/2018